MAFUNZO KWA VITENDO WANAFUNZI CHUO KIKUU ARDHI

MAFUNZO KWA VITENDO WANAFUNZI CHUO KIKUU ARDHI

Chuo Kikuu Ardhi kimekuwa kikitoa mafunzo kwa njia ya vitendo kwa sehemu kubwa kwa lengo la kuwajengea uwezo wanafunzi wao ili kuweza kuwa bora na mahiri wanapoingia kwenye soko la ajira.

Kupitia Skuli ya ubunifu majengo, usimamizi na uchumi ujenzi (SACEM|) Mhadhiri Msaidizi (assistant lecturer) Bi Oliva Gonda ameendesha sehemu ya somo lake kutoka  idara ya Sayansi ya uchumi ujenzi pamoja na wanafunzi wa  darasa hilo la mwaka wa pili juu ya mada ya aina na tabia za udongo katika ujenzi.

Wanafunzi wamepata fursa ya kutembelea maabara na kuona aina mbalimbali za udongo, vifaa mbalimbali na mashine zinazotumika kupima aina hizo na jinsi ya kuandaa udongo wa kutumika katika majenzi mbalimbali . Baadhi ya wataalamu walishirikiana na Bi Oliva kutoka Chuo Kikuu Ardhi katika kusaidia kufundisha na kuruhusu maswali mbalimbali kutoka kwa wanafunzi hao wakiwa katika maabara hiyo.

Bi Oliva alisema imekuwa ni taratibu na zoezi endelevu kwa kuwajengea uwezo wanafunzi wa kuweza kuona na hata kushiriki baadhi ya maandalizi ya vitu mballimbali ili watakapoingia sokoni wasiwe wageni na vile vitu walivyojifunza darasani.

IMG-1247

Bi Oliva Gonda Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu Ardhi akizungumza na kuwapa muongozo wanafunzi kabla ya kuingia kwenya maabara hiyo

IMG-1269

Mmmoja wa wataalamu akielezea kwa ujumla juu ya mada ya udongo ndani ya maabara.

IMG-1276

Kushoto ni Bi Oliva akiwa na wataalamu katika maabara hiyo wakiwaonesha wanafunzi baadhi ya vifaa vinavyotumika kupimia udongo

IMG-1321

Wanafunzi wakiendelea kuangalia kwa makini namna vifaa vinavyotumika katika zoezi zima la upimaji wa udongo.

IMG-1295

Baadhi ya Udongo walioweza kuona ukiwa wa aina tofauti tofauti kama zinavyoonekana kwenye picha.

IMG-1285

Mmoja wa mwanafunzi akiuliza swali kwa mtaalamu juu ya matumizi ya baadhi ya vifaa vinavyotumika kupima aina za udongo katika ujenzi.