BARAZA LA WAHITIMU CHUO KIKUU ARDHI
(ARU CONVOCATION)
Baraza la wahitimu Chuo Kikuu Ardhi limekuwa na taratibu ya kufanya kikao chake kila mwisho wa mwaka siku moja kabla ya mahafali ya Chuo kufanyika. Rais wa baraza hilo Bw. Haruna Masebu amefungua kikao hicho siku ya ijumaa taerehe 11/12/2020 katika ukumbi wa Chuo kwa kuwataka wahitimu hao na wadau mbalimbali kuonyesha juhudi katika yale yote wanayojadiliwa na kuyafanyia kazi . Hii ni moja ya mchango wa wahitimu wao kuona Chuo kinakuwa na kuzidi kufanya vizuri katika majukumu yake.
Katika baraza hili wahitimu hao walipata fursa la kupewa mada kuu mbili ikiwemo ”MANAGING UNCERTAINTY EMERGENCY SITUATION,THE STATE AND COMMNUNITY ACTION” ambayo ndio ilikuwa mada kuu ya mkutano na Mada kutoka kwa mtaalamu wa afya ”WORK AND LIFE BALANCE” iliyotolewa na Prof. Mohamed Janabi kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.
Mmmoja wa Waadhiri Wastaafu wa ARU, Dkt. Felician Komu akichangia katika mjadala wa Baraza hilo.
(kushoto) akibadilishana mawazo na Rais wa Baraza la ARU, Haruna Masebu (kulia). Pamoja nao ni Naibu Makamu Mkuu wa ARU, Profesa Gabriel Kassenga.
Wadau wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Taasis ya Jakaya Kikwete ya magonjwa ya moyo (JKCI), Prof Mohamed Janabi alipowasilisha mada.
Sehemu ya Wadau wakifuatilia mjadala uliokuwa unaendelea.