CHUO KIKUU ARDHI KUTOA ELIMU KWA JAMII
Chuo Kikuu Ardhi kupitia wataalamu wa Skuli ya Mipango Miji na Sayansi ya Jamii kwa kushirikiana na wadau kutoka Jumuiya ya Mdola ( Commonwealth Scholarships) na Shirika la Makazi Salama (SCI) kimetoa elmu kuhusu ujenzi bora wa makazi ili kujikinga na athari zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi.Elimu hiyo ilitolewa kwa wakazi wa Goba ilikuwa na lengo la kuhakikisha jamii inapata uelewa juu ya viwango na kanuni za mipango miji na matumizi bora ya ardhi.Mafunzo hayo yalitolewa siku ya jumatano Septemba 30, 2020.