CHUO KIKUU ARDHI KUSHIRIKI MAONESHO YA 15 YA ELIMU YA JUU SAYANSI NA TEKNOLOJIA

CHUO KIKUU ARDHI KUSHIRIKI MAONESHO YA 15 YA ELIMU YA JUU SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Chuo Kikuu Ardhi kimeshiriki maonesho ya 15 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika  kuanzia tarehe Agosti 31 mpaka 5 Septemba 5, 2020 katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.Chuo kimeweza kutoa taarifa na maelezo muhimu juu ya kozi na huduma mbalimbali zinazotolewa chuoni kwa wadau mbalimbali. Pia kupitia maonesho hayo wahitimu wa kidato cha sita na wadau mbalimbali waliotaka kujiunga na chuo waliweza kupata vipeperushi na kusaidiwa zoezi la udahili wa wanafunzi kwa mwaka mpya wa masomo 2020/2021.Chuo Kikuu Ardhi kimekuwa kikishiriki maonesho haya mara zote kwani imekuwa ni sehemu nzuri katika kukitangaza chuo na kutoa uelewa wa huduma mbalimbali zinazotolewa.

f00b4bcf-c733-462c-a2aa-b49ce5372492

Prof. Charles Kihampa Katibu Mtendaji Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi mara alipotembelea banda la Chuo katika maonesho ya Elimu ya Juu ya Sayansi na Teknolojia katika viwanja vya Mnazi  Mmoja Jijini Dar es Salaam.

IMG-3823(1)

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akiangalia mfano wa Uwanja wa Michezo, uliotengenezwa kutokana na Michoro iliyosanifiwa na Chuo Kikuu Ardhi, alipotembelea banda la Chuo Kikuu Ardhi katika maonesho ya 15 ya Elimu ya Juu ya Sayansi na Teknolojia ,viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam.Siku ya ufunguzi.

IMG-3530

Prof. Gabriel Kassenga Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Taaluma akiwa na Dkt. Yassin Senkondo katika banda la Chuo Kikuu Ardhi .

20200905_130523

Picha ya pamoja ya wakuu wa Vyuo mbalimbali (vyuo binafsi na serikali) walioshiriki katika maonesho ya Elimu ya Juu ya Sayansi na Teknolojia siku ya kilele ya maonesho hayo katika viwanja vya mnazi mmoja.

IMG-3550

Bw. Enock Nyakite akiwa katika banda akisaidia usajili wa wanafunzi waliotembelea banda katika maonesho hayoIMG-3780

IMG-3547

Baadhi wa wanafunzi waliotembelea Banda la Chuo Kikuu Ardhi

IMG-3560

Baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda la Chuo Kikuu Ardhi

IMG-3541

IMG-3534

IMG-4122

Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Muhimbili Prof. Andrea Pembe akiweka sahihi katika kitabu cha wageni alipotembelea banda la Chuo Kikuu Ardhi

IMG-3600