MAFUNZO KWA VITENDO WANAFUNZI CHUO KIKUU ARDHI
Chuo Kikuu Ardhi kimekuwa kikitoa mafunzo kwa njia ya vitendo kwa sehemu kubwa kwa lengo la kuwajengea uwezo wanafunzi wao ili kuweza kuwa bora na mahiri wanapoingia kwenye soko la ajira.
Kupitia Skuli ya ubunifu majengo, usimamizi na uchumi ujenzi (SACEM|) Mhadhiri Msaidizi (assistant lecturer) Bi Oliva Gonda ameendesha sehemu ya somo lake kutoka idara ya Sayansi ya uchumi ujenzi pamoja na wanafunzi wa darasa hilo la mwaka wa pili juu ya mada ya aina na tabia za udongo katika ujenzi.
Wanafunzi wamepata fursa ya kutembelea maabara na kuona aina mbalimbali za udongo, vifaa mbalimbali na mashine zinazotumika kupima aina hizo na jinsi ya kuandaa udongo wa kutumika katika majenzi mbalimbali . Baadhi ya wataalamu walishirikiana na Bi Oliva kutoka Chuo Kikuu Ardhi katika kusaidia kufundisha na kuruhusu maswali mbalimbali kutoka kwa wanafunzi hao wakiwa katika maabara hiyo.
Bi Oliva alisema imekuwa ni taratibu na zoezi endelevu kwa kuwajengea uwezo wanafunzi wa kuweza kuona na hata kushiriki baadhi ya maandalizi ya vitu mballimbali ili watakapoingia sokoni wasiwe wageni na vile vitu walivyojifunza darasani.
Continue reading MAFUNZO KWA VITENDO WANAFUNZI CHUO KIKUU ARDHI