MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU ARDHI AZUNGUMZA NA WANAFUNZI WAPYA

MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU ARDHI AZUNGUMZA NA WANAFUNZI WAPYA

Wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2020/2021 waliopata nafasi ya kujiunga na Chuo, walianza kufanyiwa makaribisho ya wiki moja  mnamo tarehe 23 Р27 Novemba,2020.

Katika wiki hiyo wanafunzi walipata nafasi ya kufanya usajili kwa kuongozwa na ofisi ya mshauri wa wanafunzi huku wakiendelea kuelekezwa mambo muhimu wanayopaswa kuwafanya  pindi wanapokuwa katika masomo yao. Mada mbalimbali zilitolewa kutoka kwa wadau nje na ndani ya chuo ili kuweza kuwasidia kufahamu vitu, mazingira na utaratibu wa Chuo. Wadau walipata nafasi hizo ni pamoja na wadau wa masuala ya afya, jinsia, mikopo, usalama, rushwa nk.

Mnamo siku ya ijumaa tarehe 27, Novemba, 2020 Prof. Evaristo Liwa Makamu Mkuu wa Chuo, alipata fursa ya kuzungumza na wanafunzi hao kwa lengo la kuwatambulisha uongozi mzima wa chuo na kuwafahamisha mambo muhimu wanapokuwa chuoni.

IMG-8868

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi akizungumza na wanafunzi siku ya hafla hiyo

Continue reading MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU ARDHI AZUNGUMZA NA WANAFUNZI WAPYA