ARU KUCHUKUA USHINDI MECHI YA KIRAFIKI
Mechi ya mpira wa miguu kati ya timu ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi na Mkongo United iliyochezwa katika viwanja vya Chuo tarehe 26 Juni, 2020 kwa lengo la kuimarisha na kujenga mahusiano mazuri kati ya ARU na Makongo.
Katika Mechi hiyo wanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi wameibuka na ushindi wa goli 3 na makongo 2. Hata hivyo Mkuu wa Idara ya michezo Bw. Boniface Tamba ameendelea kuwahimiza na kuwatengenezea mazingira ya kuwa na mechi mbalimbali za kirafiki ili kuwaimarisha wanafunzi hasa pale wanapoanza michuano ya vyuo mbalimbali isiwe ngumu kwao kufanya vizuri.