NAIBU KATIBU MKUU ARIDHISHWA NA MAANDALIZI CHUO KIKUU ARDHI

NAIBU KATIBU MKUU ARIDHISHWA NA MAANDALIZI CHUO KIKUU ARDHI.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia  Prof. James Mdoe ameridhishwa na maandalizi yaliyofanywa na Chuo Kikuu Ardhi katika kukabiliana na Maambukizi ya Virus vya Corona (COVID 19). Ameeleza hayo alipokuwa kwenye kikao kazi na Menejimenti ya Chuo alipokuja kujionea hali halisi ya maandalizi ya Chuo katika kuwapokea wanafunzi wanaorudi kwa kuanza muhula ya pili  wa masomo ulionza rasmi Juni Mosi 2020.

Wakati huo huo Makamu Mkuu wa Chuo prof. Evaristo Liwa alieleza kuwa taratibu zote za utoaji wa fedha kwa wanafunzi umekamilika hivyo wanafunzi wataingiziwa fedha kwenye akaunti zao za benki kwa wakati.

Prof. Liwa aliendelea kueleza juu ya manunuzi yalifanyika ya vifaa mbalimbali vya kujikinga na maambukizi ya Corona vikiwemo madumu,ndoo za kuhifadhia barakao zilizotumika,na vifaa maalumu kwa zahanati ya Chuo kama mavazi maalumu ya kuhudumia wagonjwa (PPE),Oxgen monitor na mask oxygen.

Pia mwishoni Naibu Katibu alipata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi wa bweni la wanafunzi lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 592 kwa wakati mmoja.

4859c3ab-a8d4-43a7-aac2-fcd5ec5b7d2b Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni  ofisini kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi.

Continue reading NAIBU KATIBU MKUU ARIDHISHWA NA MAANDALIZI CHUO KIKUU ARDHI