ARISA NA THTU WAKABIDHI BARAKOA NA VITAKASA MIKONO (SANITIZER)

ARISA NA THTU WAKABIDHI BARAKOA NA VITAKASA MIKONO (SANITIZER).

Katika kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa homa ya mapafu (COVID 19), ARISA kwa kushirikiana na THTU wamekabidhi rasmi kwa uongozi wa Chuo barakoa na vitakasa mikono kwa ajili ya wafanyakazi wa Chuo kikuu Ardhi mnamo 30, Aprili 2020.

Viongozi hao wamekabidhi vifaa hivyo kwa lengo la kusaidia uongozi wa Chuo katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona ambao umekuwa ni tishio kubwa kwa kipindi hiki.

Wakati huo huo Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Evaristo liwa ameeleza kuwa , wafanyakazi  wote Chuoni bado wanasisitizwa kufuata mwongozo uliotolewa na Wizara ya afya hivi karibuni pamoja na mambo mengine yanayosisita kunawa mikono mara kwa mara kwa maji yanayotirirka na sabuni,kuvaa barakoa na kukaa umbali wa mita moja kati ya mtu na mtu.

”Corona Inaepukika ,Chukua tahadhari”

IMG-7192(1)

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Prof. Evaristo Liwa akitoa neno la shukrani wakati akipokea vifaa hivyo ofisini kwake. Continue reading ARISA NA THTU WAKABIDHI BARAKOA NA VITAKASA MIKONO (SANITIZER)