CHUO KIKUU ARDHI CHAJINYAKULIA VIKOMBE NANE VYA USHINDI KATIKA MASHINDANO YA TUSA

CHUO KIKUU ARDHI CHAJINYAKULIA MEDALI 18 NA VIKOMBE NANE VYA USHINDI KATIKA MASHINDANO YA TUSA

Chuo Kikuu Ardhi kimeshinda medali 18 na vikombe nane katika mashindano ya michezo mbalimbali yaliyoshirikisha Vyuo Vikuu Nchini maarufu TUSA.

Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi vikombe kwa uongozi wa Chuo, Mwalimu wa michezo wa Chuo Kikuu Ardhi Bw. Boniface Tamba amesema Chuo kimepata vikombe baada ya kuibuka washindi kwenye michezo ya mpira wa kikapu, mpira wa meza, scrabble, chess na kuogelea.

Naye Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala Prof. Carolyne Nombo amewapongeza wachezaji wote kwa ushindi na kuwataka kuongeza juhudi ili waweze kuibuka washindi wa kwanza kwenye michezo yote watakayoshiriki.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Evaristo Liwa amewataka ofisi ya michezo kuzingatia mashindano ya ndani (Inter University Competition) ili kuweza kuibua vipaji zaidi vya wanamichezo ambao watakiwakilisha vema Chuo katika mashindano mengine. Kwa kipekee amempongeza mwanadada Digna Mugishangwe kwa kuibuka mshindi kwenye vipengele vyote vya kuogelea vilivyoshindanishwa na hivyo kujinyakulia kikombe na medali 12.

IMG_9820Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala Prof. Carolyne Nombo akitoa neno fupi kabla ya kumkaribisha Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Evaristo Liwa. Continue reading CHUO KIKUU ARDHI CHAJINYAKULIA VIKOMBE NANE VYA USHINDI KATIKA MASHINDANO YA TUSA