CHUO KIKUU ARDHI CHATOA SEMINA ELEKEZI KWA WAAJIRIWA WAPYA

CHUO KIKUU ARDHI CHATOA SEMINA ELEKEZI KWA WAAJIRIWA WAPYA

Chuo Kikuu Ardhi chatoa semina elekezi kwa waajiriwa wapya katika maswala mbalimbali yahusuyo ajira zao ili kuleta tija na ufanisi kazini.

Akizungumza na wafanyakazi hao, Prof. Carolyne Nombo ambaye ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala amesema, Chuo kimekua kikiandaa utaratibu wa kuwakutanisha wafanyakazi wapya na uongozi wa Chuo pamoja na maafisa waandamizi mbalimbali ili kuwajengea uelewa wa mambo mbalimbali muhimu kwa utendaji  kazi wao. Pia amewataka Waajiriwa hao kusoma sera na miongozo mbalimbali ya Chuo ili kuweza kuelewa vyema haki zao na wajibu wao kwa taasisi na taifa kwa jumla.

Akifungua mafunzo hayo ya siku moja, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Gabriel Kassenga amewaasa wafanyakazi kuwa wazalendo kwa taasisi yao na kujitolea kufanya kazi zinazohusu ustawi wa Chuo pindi watakapohitajika kufanya hivyo. Pia amewataka waajiriwa wanataaluma kujiendeleza zaidi kielimu, kufanya tafiti na kutoa machapisho ili kuendelea kupanda kitaaluma na pia kuifanya hadhi ya Chuo kuendelea kupanda.

IMG_1910

Prof. Carolyne Nombo akitoa neno kabla ya kumkaribisha Kaimu Makamu Mkuu wa Prof. Gabriel Kassenga kufungua na kuongea na wanataaluma. Continue reading CHUO KIKUU ARDHI CHATOA SEMINA ELEKEZI KWA WAAJIRIWA WAPYA