JUMUIYA YA CHUO KIKUU ARDHI KUSHIRIKI BONANZA LA MICHEZO.
Chuo Kikuu Ardhi chini ya Idara ya Michezo kwa kushirikiana na uongozi wa Chuo Kikuu Ardhi waliandaa bonanza na michezo kwa wanajumuiya wa Chuo Kikuu Ardhi siku ya Tarehe 28. 6. 2019 katika viwanja vya Chuo Kikuu Ardhi.Bonanza hilo lilihusisha wafanyakazi na wanafunzo wote wa Chuo Kikuu Ardhi kwa kuandaa michezo na mbali mbali ikiwemo mazoezi ya viungo, kula apple, kukimbia,mpira wa miguu, mpira wa kikapu na kuvuta kamba.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Prof. Gabriel Kassenga alifungua rasmi zoezi hilo na kushiriki kuangalia baadhi ya michezo iliyoandaliwa na idara hiyo. Prof. G. Kassenga pia shiriki kuangalia mashindano ya michezo mbalimbali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi na kukabidhi zawadi kwa washindi wote walioshiriki na kuweza kutoka na ushindi katika michezo hiyo ikiwemo timu za wanafunzi na baadhi ya wafanyazi walioshiriki michezo hiyo.
Prof. Kassenga ambaye alikuwa ni ngeni rasmi katika bonanza hilo alipata nafasi ya kuzumza na wafanyakazi na wanafunzi walioshiriki zoezi hilo kwa kuwataka wawe wanajitokeza kwa wingi kwenye mazoezi na machizo mbalimbali inayoandaliwa na Chuo kwa lengo la kujenga mahusiano mahala pa kazi. Continue reading JUMUIYA YA CHUO KIKUU ARDHI KUSHIRIKI BONANZA LA MICHEZO