ARU “Educates” service providers about HIV/AIDS and other Sexual transmitted diseases


ARU “Educates” service providers about HIV/AIDS and other Sexual transmitted diseases

Ardhi University Dispensary conducted a seminar on HIV/AIDS and Sexual transmitted diseases to educate ARU service providers. During the seminar there were also voluntary HIV testing and counseling service which provided by ARU Dispensary staff.

BLOG 7
Continue reading ARU “Educates” service providers about HIV/AIDS and other Sexual transmitted diseases

KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII YARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UKARABATI CHUO KIKUU ARDHI

KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII YARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UKARABATI CHUO KIKUU ARDHI 

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imeipongeza serikali kwa kutoa fedha kiasi cha shilingi bilioni 2.5 za mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya Chuo Kikuu Ardhi zilizotengwa katika  bajeti ya mwaka 2018/19.

Pongeza hizo zimetolewa na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Oscar Mukasa (MB) Jijini Dar es Salaam baada ya kukagua utekelezaji wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu hiyo ambayo ni ujenzi wa maabara, ukarabati wa karakana, nyumba za walimu, madarasa na kukamilisha ujenzi wa jengo la lands.

Aidha, Mhe. Mukasa pamoja na Kamati wameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kusimamia utekelezaji wa mradi kwa ubora na weledi mkubwa.Vilevile wamepongeza Chuo Kikuu Ardhi kwa kutumia vyema wataalamu wake kwenye kutekeleza kazi ya ujenzi.

Katika hatua nyingine kamati imeshauri Serikali kutoa kipaumbele cha kukiendeleza kituo cha utoaji taarifa za viashiria vya majanga yanayoweza kusababishwa na Volcano na matetemeko ya ardhi katika eneo la OldonyoLengai. Aidha wameishauri Serikali kuhakikisha Kituo kinapata vifaa vitakavyokiwezesha kufanya kazi ya kutambua viashiria hivyo katika maeneo yote ya nchi na kutoa taarifa hizo.

Awali Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Prof. Evaristo Liwa, akitoa taarifa ya utekelezaji kwa kamati amesema mradi huo unaogharimu Shilingi Bilioni 2.5 kwa kiasi kikubwa umesimamiwa na wataalamu wa ndani ya Chuo hali ambayo imewezesha kupunguza gharama na ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha kwa wakati .

Nae Waziri Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameishukuru Kamati hiyo kwa kutembelea mradi na ameahidi kusimamia kwa ukaribu utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na kamati.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano

Chuo Kikuu Ardhi

15/3/2019

PI

 

 

 

 

 

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako wakibadilishana mawazo na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Oscar Mukasa (MB) wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya Chuo Kikuu Ardhi. Continue reading KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII YARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UKARABATI CHUO KIKUU ARDHI

WAKUU WA IDARA, WATENDAJI NA WAJUMBE WA KAMATI WAFAIDIKA NA MAFUNZO YA UELEWA WA MAAFA NA JITIHADA ZA KUYAPUNGUZA

WAKUU WA IDARA, WATENDAJI NA WAJUMBE WA KAMATI WAFAIDIKA NA MAFUNZO YA UELEWA WA MAAFA NA JITIHADA ZA KUYAPUNGUZA

Wakuu wa Idara, watendaji na wajumbe wa kamati ya maafa jijini Tanga wapewa mafunzo ya uelewa wa maafa na jitihada za kuyapunguza katika ngazi ya Halmashauri ya jiji la Tanga.

1Naibu Makamu Mkuu wa Chuo -Taaluma Prof. Gabriel Kassenga akitoa utangulizi kuhusu mafunzo ya uelewa wa maafa na jitihada za kuyapunguza katika ngazi ya Halmashauri. Continue reading WAKUU WA IDARA, WATENDAJI NA WAJUMBE WA KAMATI WAFAIDIKA NA MAFUNZO YA UELEWA WA MAAFA NA JITIHADA ZA KUYAPUNGUZA

WANAWAKE CHUO KIKUU ARDHI WAADHIMISHA SIKU YAO KWA KUWASHIKA MKONO WATOTO WENYE SARATANI DAR

WANAWAKE CHUO KIKUU ARDHI WAADHIMISHA SIKU YAO KWA KUWASHIKA MKONO WATOTO WENYE SARATANI DAR

1T4A4826Sehemu ya Wanawake wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakishiriki maandamano katika siku ya maadhimisho ya wanawake duniani. Maandamano yalianzia Chuoni hapo na kuhitimishwa eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam. Continue reading WANAWAKE CHUO KIKUU ARDHI WAADHIMISHA SIKU YAO KWA KUWASHIKA MKONO WATOTO WENYE SARATANI DAR