MAHAFALI YA 12 YA CHUO KIKUU ARDHI (ARU) YAFANA

MAHAFALI YA 12 YA CHUO KIKUU ARDHI (ARU) YAFANA

GR6Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi, Profesa Evaristo Liwa akimkaribisha Mkuu wa Chuo, Mhe. Cleopa David Msuya katika mahafali ya 12 ya Chuo Kikuu Ardhi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 1 Disemba 2018. Kulia ni Mwenyekiti Mpya wa Baraza la Chuo, Balozi Prof. Costa Mahalu na viongozi waandamizi wa ARU.  Continue reading MAHAFALI YA 12 YA CHUO KIKUU ARDHI (ARU) YAFANA

WANAFUNZI BORA WA CHUO KIKUU ARDHI WAPEWA TUZO NA ZAWADI ZAO

WANAFUNZI BORA WA CHUO KIKUU ARDHI WAPEWA TUZO NA ZAWADI ZAO

Novemba 30 2018 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi, Profesa Evaristo Liwa alikabidhi zawadi kwa wanafunzi 98 waliofanya vyema katika masomo. Kati ya hao wasichana ni 51 sawa na asilimia 52 ya wanafunzi wote waliopata tuzo na wavulana ni  47 sawa na asilimia 48 ya wanafunzi wote ambao wamefuzu na kupata tuzo na zawadi mbalimbali kwa vipengele mbalimbali vya kitaaluma. Aidha Profesa Liwa amewapongeza wanafunzi wanaohitimu Desemba Mosi na wote waliojinyakulia zawadi mbalimbali kwa kuendeleza kuweka juhudi katika masomo kwa kipindi chote walichokuwa chuoni.

12Mwanafunzi Bora wa Jumla wa Chuo Kikuu Ardhi, Arnold Mushi akikabidhiwa vyeti na Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Evaristo Liwa wakati wa hafla ya kukabidhi wanafunzi 98 vyeti katika viwanja vya Chuo.
Continue reading WANAFUNZI BORA WA CHUO KIKUU ARDHI WAPEWA TUZO NA ZAWADI ZAO