ARDHI UNIVERSITY STUDENT PARTICIPATE ON THE 19TH WORLD FESTIVAL OF YOUTH AND STUDENTS.

ARDHI UNIVERSITY STUDENT PARTICIPATE ON THE 19TH WORLD FESTIVAL OF YOUTH AND STUDENTS SOCHI.

Nicodemus David Agweyo, Ardhi University students from the school of Real Estate Studies participated on the 19th world festival of youth and students SOCHI for the aim of discussing issues about sustainable development goals,looking on it’s implementation and challenges towards its execution.Further more had discussion on the Cultural,Economy,Technology,Environment , Politics and it’s effectiveness in regional,country wide and global at large.Other participant from Tanzania University were from University of Dar es Salaam,St.Augustine,Kairuki University and ARU.The event  held on 12 -23 of October 2017 in Russia.

pic

Nicodemus David Agweyo Ardhi University students taking  BSC in Land Managemet and Valuation at Russia.

Continue reading ARDHI UNIVERSITY STUDENT PARTICIPATE ON THE 19TH WORLD FESTIVAL OF YOUTH AND STUDENTS.

Chuo kikuu Ardhi chahimizwa kutumia wanataaluma wake kutatua changamoto za Ardhi nchini.

Chuo kikuu Ardhi chahimizwa kutumia wanataaluma wake kutatua changamoto za Ardhi nchini.

Chuo kikuu Ardhi kimetakiwa kutumia wanataaluma wake kuelekeza nguvu kubwa katika kukabiliana na changamoto na kutatua matatizo ya ardhi ambayo yanaathiri kwa kiasi kukubwa jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano ya kufufua uchumi kupitia mpango wa “Tanzania ya Viwanda” unaolenga kuipelekea Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo 2025.

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati wa ufunguzi wa mradi wa kituo cha mtandao wa utawala bora katika sekta ya ardhi ukanda wa nchi za afrika mashariki (Network of Excellence in Land Governance in Africa, Eastern Africa) uliofanyika chuoni hapo ijumaa hii Oktoba 27, 2017.

Akizungumza kuhusu nafasi ya chuo hicho katika kuendeleza sekta ya Ardhi nchini, Lukuvi amesema chuo hicho ndio chuo pekee kinachozalisha wataalam katika sekta ya ardhi ambapo umefika wakati sasa wa kijitathmini ni kwa kiasi gani kimeweza kuchangia katika kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta ya ardhi.

“Sote tunatambua kuwa kuna changamoto nyingi za kiutendaji katika sekta ya ardhi. Ni mategemeo yangu kuwa kupitia mradi huu ambao ninauzindua leo wa kituo cha mtandao wa utawala bora katika sekta ya ardhi ukanda wa nchi za afrika mashariki (NELGA – Eastern Efrica Node), Chuo kama taasisi yenye wataalamu waliobobea kwenye fani za ardhi, kitatoa mchango mkubwa katika kukabiliana na changamoto hizi” alisema Mhe. Lukuvi.

Awali akitoa maelezo kuhusu mradi wa NELGA, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi, Prof. Evaristo Liwa alisema upatikanaji wa mradi huu katika Chuo Kikuu Ardhi ni matokeo ya ubobezi na uwezo wa chuo hiki katika masuala mbalimbali yanayoizunguka ardhi ambapo April 2016 kilichaguliwa na Umoja wa nchi za Afrika (AU) kupitia mradi wa “NELGA” (Network of Excellence in Land Governance in Africa, Eastern Africa) ili kuhudumia kama kitovu cha kuboresha mtandao wa elimu na mafunzo katika sekta ya ardhi “NELGA node” ukanda wa nchi Afrika Mashariki.

Fursa ambayo pia ilipelekea Chuo kupata ufadhili wa kuanzisha mradi wa kuboresha usimamizi katika sekta ya Ardhi kutoka Serikali ya Ujerumani. Ufadhili huu ulitokana na tafiti zilizofanywa na Umoja wa Nchi za Africa (African Union) kupitia kituo cha Mpango wa Sera ya Ardhi (The Land Policy Initiative – LPI) na kubainisha taasisi za kitaaluma bobezi katika masuala ya ardhi na mazingira ambapo pia ilibainishwa kuwepo kwa mapungufu katika utendaji kwa wataalamu wa sekta ya Ardhi katika Afrika.

Prof. Liwa alisema ili kufanikisha utekelezaji wa program hii Bara la Afrika limegawanywa katika kanda 5 mojawapo ikiwa ni Kanda ya Mashariki ya Afrika. Chuo Kikuu Ardhi kimechaguliwa kusimamia utekelezaji wa program hiyo katika ukanda huu ambapo Mradi huu unalenga kutekeleza Kukuza taaluma kwa kutoa ufadhili kwa wanafunzi wanaochukua shahada za uzamili, Kuwezesha ubadilishanaji wa wanataaluma kwenye vyuo vishiriki kwenye mradi, Kutoa elimu na mafunzo kuziba mianya iliyoonekana katika tafiti zilizofanywa na Mpango wa Sera ya Ardhi (Land Policy Initiative), Kuchangia uboreshaji wa sera za ardhi katika nchi zinazoshiriki kwenye mradi na Kuanzisha mchakato wa ukusanyaji na utunzaji wa taarifa zinazohusu masuala ya ardhi katika Maktaba ya Chuo Kikuu Ardhi .

Mradi huu wa NEGLA ambapo ni sehemu ya ufadhili wa Serikali ya Ujerumani kupitia Shirika lake la Maendeleo (GIZ) katika awamu hii ya kwanza ambayo imepangwa kutekelezwa katika kipindi cha miezi 18 kuanzia Agosti 2017 na imepanga kutumia jumla ya Euro 230,000. Pamoja na wageni wengine uzinduzi huu ulihudhuliwa pia na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) nchini Tanzania, Bw. Ernst Hustaedt

NO. 2Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Prof. Evaristo Liwa kabla ya uzinduzi wa mradi wa kituo cha mtandao wa utawala bora katika sekta ya ardhi ukanda wa nchi za Afrika Mashariki. Continue reading Chuo kikuu Ardhi chahimizwa kutumia wanataaluma wake kutatua changamoto za Ardhi nchini.

WAFANYAKAZI WA CHUO KIKUU ARDHI KUPEWA ELIMU JUU YA UZIMAJI MOTO

WAFANYAKAZI  CHUO KIKUU ARDHI KUPEWA ELIMU JUU YA UZIMAJI MOTO

UONGOZI WA CHUO KIKUU ARDHI UMEANDAA MAFUNZO YA SIKU MBILI JUU YA ELIMU WA UZIMAJI MOTO KWA LENGO LA KUSAIDIA KUJIKINGA NA MAJANGA YA MOTO KATIKA MAENEO YA KAZI. WASHIRIKI NI WAFANYAKAZI WOTE WA CHUO KIKUU ARDHI,ZOEZI HILI LIMEFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA CHUO KIKUU ARDHI TAREHE 18 NA 19 OCTOBA,2017.

MOTO 1

Baadhi ya wafanyakazi katika mafunzo ya moto kwenye viwanja vya Chuo Continue reading WAFANYAKAZI WA CHUO KIKUU ARDHI KUPEWA ELIMU JUU YA UZIMAJI MOTO

SHIMUTA BONANZA MKOA WA DAR ES SALAAM KUFANYIKA VIWANJA VYA CHUO KIKUU ARDHI.

 SHIMUTA BONANZA MKOA WA DAR ES SALAAM KUFANYIKA VIWANJA VYA CHUO KIKUU ARDHI.

Chuo Kikuu Ardhi kwa kushirikiana na wafanyakazi wengine wa Taasisi za umma wamejumuika pamoja katika viwanja vya Chuo Kikuu Ardhi siku ya Jumamosi tarehe 14/10/2017 kufanya mashindano ya michezo mbalimbali yakiwemo mazoezi ya viungo, mpira wa miguu, mpira wa kikapu, kukimbia kwenye gunia, kukimbiza kuku nk. Kwa lengo la kuzindua SHIMUTA  itakayofanyika mkoani Iringa mwezi Novemba mwaka huu.Taasisi za umma zilizoshiriki ni pamoja na Bodi ya Mikopo,TBS, TPDC, TANESCO, UDSM, NEMC, CBE, IFM n.k. Bonanza hilo lilifunguliwa rasmi na Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo Bw.Yusuph Singo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

      1Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo Bw.Yusuph Singo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akiongea na washiriki wa Bonanza wakati wa ufunguzi katika viwanja vya Chuo Kikuu Ardhi. Continue reading SHIMUTA BONANZA MKOA WA DAR ES SALAAM KUFANYIKA VIWANJA VYA CHUO KIKUU ARDHI.