CHUO KIKUU ARDHI CHATEKELEZA AGIZO LA SERIKALI LA KUFANYA MAZOEZI KILA JUMAMOSI YA PILI YA MWEZI
Katika kutekeleza agizo la serikali la kuwataka wananchi kufanya mazoezi ya viungo kila Jumamosi ya pili ya mwezi, uongozi wa Chuo Kikuu Ardhi ikishirikiana na Idara ya michezo iliandaa mazoezi ya viungo yaliyofanyika katika viwanja vya ARU ambapo yalitanguliwa na matembezi ya umbali wa kilomita tatu (3) yalioanzia jengo la Utawala la Chuo Kikuu Ardhi kuzunguka maeneo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mazoezi hayo yaliongozwa na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Gabriel Kassenga sambamba na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo -Mipango, Fedha na Utawala Prof. Evaristo Liwa.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Gabriel Kassenga (katikati) kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo -Mipango, Fedha na Utawala Prof. Evaristo Liwa, kushoto ni Mkufunzi wa Michezo Bw. Boniface Tamba. Continue reading CHUO KIKUU ARDHI CHATEKELEZA AGIZO LA SERIKALI LA KUFANYA MAZOEZI YA VIUNGO KILA JUMAMOSI YA PILI YA MWEZI →