MASHINDANO YA INTERSCHOOL YAMEANZA RASMI CHUO KIKUU ARDHI

MASHINDANO YA INTERSCHOOL YAMEANZA RASMI CHUO KIKUU ARDHI

Mashindano ya Skuli  zote za Chuo Kikuu Ardhi yameanza rasmi tarehe 03/07/2020 ambayo yanahusisha aina mbalimbali za michezo ikiwepo mpira wa miguu, mpira wa kikapu na mingine.  Bi. Amina Mdidi Mshauri wa wanafunzi alifungua rasmi mashindano hayo kwa mechi ya ufunguzi kati ya SACEM na SSPSS ambapo mchuano huo walitoka sare kwa goli 1 kwa 1.

IMG-9449

Bi. Amina Mdidi akikagua timu hizo kabla ya kuanza rasmi mpira huo

Continue reading MASHINDANO YA INTERSCHOOL YAMEANZA RASMI CHUO KIKUU ARDHI

PROF.EVARISTO LIWA AZUNGUMZA NA UONGOZI MPYA WA ARUSO

PROF. EVARISTO LIWA AZUNGUMZA NA UONGOZI MPYA WA ARUSO

Prof. Evaristo Liwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi amezungumza na uongozi mpya wa serikali ya wanafunzi ARUSO unaingia madarakani rasmi kwa mwaka 2020/2021. Prof. Liwa alipata nafasi ya kuzungumza na uongozi huo mpya siku ya tarehe 30 Juni,2020 alipohudhuria hafla fupi ya makabidhiano ya viongozi wanaomaliza muda wao na wanaoingia madarakani.

 Halfa hiyo huwa hufanyika kila mwaka pale uongozi mpya unapotaka kuingia madarakani ambayo huandaliwa na  na ofisi ya Mshauri wa wanafunzi kwa lengo la kushuhudia na kuweza kupata maneno ya kujenga kutoka kwa viongozi wa Chuo.

Sambamba na hilo Prof Liwa akiwa ni mgeni rasmi ya halfa hiyo aliueleza uongozi mpya kuwa nafasi walizopewa wanapaswa kuwajibika kila mmoja kwa nafasi yake na kuhakikisha wanashirikiana vizuri na uongozi wa chuo katika utendaji wao.Aliendelea kusema kuna vitu vingi vya msingi vya kufuatilia kama usajili wa wanafunzi,kufuata sheria ziliwekwa na chuo,na kulipa ada kwa wakati ili kusaidia kuondoka changamoto mbalimbali hapa chuoni.

Continue reading PROF.EVARISTO LIWA AZUNGUMZA NA UONGOZI MPYA WA ARUSO

ARU KUCHUKUA USHINDI MECHI YA KIRAFIKI

ARU KUCHUKUA USHINDI MECHI YA KIRAFIKI

Mechi ya mpira wa miguu kati ya timu ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi na Mkongo United iliyochezwa katika viwanja vya Chuo tarehe 26 Juni, 2020 kwa lengo la kuimarisha na kujenga mahusiano mazuri kati ya ARU na Makongo.

Katika Mechi hiyo wanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi wameibuka na ushindi wa goli 3 na makongo 2. Hata hivyo Mkuu wa Idara ya michezo Bw. Boniface Tamba ameendelea kuwahimiza na kuwatengenezea mazingira ya kuwa na mechi mbalimbali za kirafiki ili kuwaimarisha wanafunzi hasa pale wanapoanza michuano ya vyuo mbalimbali isiwe ngumu kwao kufanya vizuri.

1ce048fe-25d6-43a4-9954-1503f08494c3

Continue reading ARU KUCHUKUA USHINDI MECHI YA KIRAFIKI

MAFUNZO KWA VITENDO KWA WANAFUNZI CHUO KIKUU ARDHI

MAFUNZO KWA VITENDO KWA WANAFUNZI CHUO KIKUU ARDHI.

Wanafunzi Chuo Kikuu Ardhi wamekuwa wakifanya mafunzo kwa viendo kama taratibu na miongozo ya kuwawezesha kuimarika zaidi kwa yale wanayofundishwa darasani .Hii imekuwa moja ya chanzo cha kuwaandaa wanafunzi hawa ili wanapohitimu masomo yako wanakuwa wenye uwelewa mkubwa kwa yale wanayofundishwa darasani.

Kila upimaji unaanza na alama rejea (reference points).Pichani ni baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa pili wa Shahada ya Geomatics na Geoinformatics wakiandaa alama za msingi ambazo  msingi(control points) ambazo  watazitumia kama alama rejea ikiwa ni sehemu ya mafunzo ya upimaji unaopelekea umiliki wa ardhi (cadastral surveys).

7e4840d2-8235-4c02-80e4-033c9bf00d27

Wanafunzi wakiwa katika mafunzo kwa vitendo.

Continue reading MAFUNZO KWA VITENDO KWA WANAFUNZI CHUO KIKUU ARDHI

TAHADHARI DHIDI YA MAAMBUKIZI YA CORONA

TAHADHARI DHIDI YA MAAMBUKIZI YA CORONA

web covid

Uongozi wa Chuo Kikuu Ardhi kwa kushirikiana na Zahanati ya Chuo wanaendela kuwakumbusha wanajumuiya wote wa Chuo kuendelea kuzingatia mambo ya muhimu katika kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 ( Corona) wanapokuwa eneo la Chuo.

TUNAENDELEA KUCHUKUA TAHADHARI CHUONI

TUNAENDELEA KUCHUKUA TAHADHARI CHUONI

wanafunzi

Katika kuendelea kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 wanafunzi Chuo Kikuu Ardhi wameendelea kuchukua tahadhari wanapokuwa Chuoni kwa kunawa mikono, kuvaa barakoa na kuzingatia umbali. Kama wanavyoonekana Pichani wakiwa katika mazingira ya Chuo wakiendelea na masomo.

KUREJEA KWA MICHEZO KATIKA VIWANJA VYA CHUO KIKUU ARDHI

KUREJEA KWA MICHEZO KATIKA VIWANJA VYA CHUO KIKUU ARDHI

Tangazo michezo

Idara ya Michezo Chuo Kikuu Ardhi inapenda kuwakumbusha wanajumuiya wote kuwa shughuli za michezo zinazofanyika katika viwanja vya chuo zimeruhusiwa kufanyika kuanzia tarehe 1/06/2020.

Pia bado inakumbushwa kuendelea kufuata taratibu zinazopaswa kuzingatiwa na wanamichezo muda wote wanapokuwepo viwanjani, kunawa mikono na maji tiririka na sabuni kabla na baada ya michezo,wachezaji hawaruhusiwi kucheza au kufanya mazoezi huku wamevaa barakoa,watazamaji wote wanatakiwa kuvaa barakoa n akuzingatia umbali wa mita moja na pia wanamichezo wote hawaruhusiwi kuingia na magari yao maeneo ya viwanja vya michezo,magari yote yaachwe sehemu husika za maegesho yanayoruhusiwa.

”Tuendelee kuchukua tahadhari,Corona inaepukika”